Teremsha Bunduki Lyrics by Roma Mkatoliki

1 week ago 4

Roma Mkatoliki Lyrics

Teremsha Bunduki is simply a liberation opus by Tanzanian rapper Roma Mkatoliki, known for his politically conscious and socially charged music.

teremsha bunduki screen

Read and bask Teremsha Bunduki Lyrics by Roma below:

Intro
Afande teremsha bunduki
Unawatetea mbona hawakukumbuki
Unatuonea, unatupiga mabuti
Mara virungu, mara unataka kutushuti

Chorus
Afande teremshaa! Hai! Hai hai!
Afande teremsha bunduki! Hai hai!
Afande teremshaa! Hai! Hai hai!
Afande teremsha bunduki! Hai hai!
Afande teremshaa! Hai! Hai hai!
Afande teremsha bunduki! Hai hai!
Afande teremshaa! Hai! Hai hai!
Afande teremsha bunduki! Hai hai!

Stanza One
Anayeandamana, hana sindano wala kiwembe
So kumuua muandamaji sio ushujaa, huoni uzembe
Mnabeba silaha nzito, akili zenu zisiwe nyepesi
Jeshi ni wito, sio muujiza wa kupuliza gesi

Nyie mnavunja amani
Mnapiga raia mahakamani
Mwisho wapoteze imani
Waamue kumalizana mtaani

Hamuheshimu muhimili
Nyie makatili
Hamna maadili
Hamstahili Injili
Labda albadili
Tena alfajiri

Wanaofaidika bosi zenu, sio nyie askari wa chini
Kwa posho ndogo mnatumwa mtupige, sasa kwanini?
Yaani unamuua anayepambania kesho bora ya mwanao
Huku unamlinda anayekuibia, na ukistaafu hakupi mafao

Watoto wao wana mali
Wanaendesha Bugatti, Ferrari
We askari njaa kali
Unadaiwa kwa mangi sukari

Na hauna gari, tu unagombea mwendokasi hatari
Tukidai mabasi, unapiga risasi
We ndio muasi

Chorus
Afande teremshaa! Hai! Hai hai!
Afande teremsha bunduki! Hai hai!
Afande teremshaa! Hai! Hai hai!
Afande teremsha bunduki! Hai hai!
Afande teremshaa! Hai! Hai hai!
Afande teremsha bunduki! Hai hai!
Afande teremshaa! Hai! Hai hai!
Afande teremsha bunduki! Hai hai!

Stanza Two
Unayemuona adui unampiga, ndio anayekulipa mshahara
Ndio mwalimu wa mwanao, ndio nesi aliyekufanyia tohara
Ungana nasi, hizo bunduki sio za kumlinda mtawala
Anayetuibia na kututeka huku akihubiri 4 R

Tuna jobless laki tano, anaahidi ajira elfu saba
Na mnashingilia Oktoba, mtatiki, mtapigwa mnada
Kama ameshindwa miaka minne, ndio ataweza siku mia?
Kafeli bima, mnadanganywa kitoto, nawahurumia

Hawaheshimu hata wajumbe, ndio chanzo cha hizi vurugu
Maana wanapitisha wabunge ambao wanaweza kuwamudu
Tusiruhusu huu uchaguzi, ni uchafuzi, na ulanguzi wa kipuuzi
Mashuzi, wamelose fuse, wamekata pumzi

Chorus (Outro)
Afande teremsha bunduki
Unawatetea mbona hawakukumbuki
Unatuonea, unatupiga mabuti
Mara virungu, mara unataka kutushuti

Afande teremshaa! Hai! Hai hai!
Afande teremsha bunduki! Hai hai!
Afande teremshaa! Hai! Hai hai!
Afande teremsha bunduki! Hai hai!
Afande teremshaa! Hai! Hai hai!
Afande teremsha bunduki! Hai hai!
Afande teremshaa! Hai! Hai hai!
Afande teremsha bunduki! Hai hai!

Check Lyrics of latest songs here, and get caller updates arsenic they driblet via X and Facebook

Read Entire Article